Ni kitabu chenye hazina ya tungo zilizotungwa na mtunzi mahiri aliyebobea katika fani ya utunzi wa mashairi, tenzi, ngonjera na nyimbo. Mtunzi wa kitabu hiki amejumuisha tungo alizozitunga hivi karibuni na zile alizozitunga kitambo nyuma hivyo kikifanya kitabu hiki kiwe na hisia tofauti tofauti. Tofauti na vitabu vingine ama watunzi wengine, upekee wa kitabu hiki ni kwamba, mtunzi wake ameonyesha umahiri wa kucheza na lugha kwa kuchanganya maneno ya Kiswahili sanifu, Kiswahili cha mitaani na maneno aliyoyatohoa katika ...
Read More
Ni kitabu chenye hazina ya tungo zilizotungwa na mtunzi mahiri aliyebobea katika fani ya utunzi wa mashairi, tenzi, ngonjera na nyimbo. Mtunzi wa kitabu hiki amejumuisha tungo alizozitunga hivi karibuni na zile alizozitunga kitambo nyuma hivyo kikifanya kitabu hiki kiwe na hisia tofauti tofauti. Tofauti na vitabu vingine ama watunzi wengine, upekee wa kitabu hiki ni kwamba, mtunzi wake ameonyesha umahiri wa kucheza na lugha kwa kuchanganya maneno ya Kiswahili sanifu, Kiswahili cha mitaani na maneno aliyoyatohoa katika lugha nyingine mbalimbali ambayo hutumiwa kwa wingi katika jamii ya sasa, na ndio sababu hasa amekiita kitabu hiki "Mashairi ya Kisasa" Burudani kamili inapatikana ndani ya kitabu hiki katika sehemu ya malumbano ambapo mtunzi wa kitabu hiki amejibizana na washairi wengine waliobobea wakiwemo Shehe Hadji Saeedia, Stephen S. Mkoloma, Sharifa Bakari, Linda Ndalu, Ndugu Chilewa, Omari Njenje na Ndugu Mgimba. Kama ilivyo ada yake, katika kurasa za mwisho wa kitabu hiki mwandishi ameweka kamusi ya Kiswahili cha mitaani ili kila asomaye kitabu hiki apate burudani kamili asomapo ama aimbapo tungo zake.
Read Less
Add this copy of Nimebadilika 2011: Mashairi + Malumbano ya Kisasa to cart. $17.45, new condition, Sold by Ingram Customer Returns Center rated 5.0 out of 5 stars, ships from NV, USA, published 2011 by iUniverse.
Add this copy of Nimebadilika 2011: Mashairi + Malumbano Ya Kisasa to cart. $36.63, good condition, Sold by Bonita rated 4.0 out of 5 stars, ships from Newport Coast, CA, UNITED STATES, published 2011 by iUniverse.