Kujifunza kuongea Kiingereza sanifu hakuna mwisho. Ili kuendeleza kujua sarufi za lugha ya Kiingereza ni lazima kwanza ujue misingi ya kweli ya sarufi hizo. Vitabu vingi vya kufundisha lugha mbalimbali huwa vinachosha - hiki hapa hakishoshi. Vitabu vya darasani havitaweza kukusaidia kujifunza Kiingereza sanifu cha kawaida ambacho ndicho unahitajika kujua. Unahitaji kujifunza Kiingereza halisi kinachoongelewa na watu wanaotumia lugha hii kama kile kinachotumika kwenye televisheni na radio. Kitabu hiki kimeandikwa na mtu ...
Read More
Kujifunza kuongea Kiingereza sanifu hakuna mwisho. Ili kuendeleza kujua sarufi za lugha ya Kiingereza ni lazima kwanza ujue misingi ya kweli ya sarufi hizo. Vitabu vingi vya kufundisha lugha mbalimbali huwa vinachosha - hiki hapa hakishoshi. Vitabu vya darasani havitaweza kukusaidia kujifunza Kiingereza sanifu cha kawaida ambacho ndicho unahitajika kujua. Unahitaji kujifunza Kiingereza halisi kinachoongelewa na watu wanaotumia lugha hii kama kile kinachotumika kwenye televisheni na radio. Kitabu hiki kimeandikwa na mtu ambaye alipata elimu yake ya awali na ya kati katika shule za umma, hivyo alijifunza vizuri kuongea Kiingereza the hard way - kwa kujaribu kujifunza siri nyingi ambazo hazielezwi na walimu wa lugha hii ya Kiingereza. Kitabu hiki kinawapa watu wanaoongea Kiswahili maarifa ya zaidi yatakayokusaidia kuongea Kiingereza mapema, vizuri na bila kuwa na makosa mengi. Kitabu hiki cha Sarufi kitakupa mwanga na utambulishio wa mambo mbalimbali ya sarufi za lugha ya Kiingereza. Pauline Mandari amegusa mambo kadhaa ya muhimu kuanzia jina, kiwakilishi nomino, vielezi, vivumishi, vishirikishi, vitenzi, viunganishi, jinsi ya kuunda sentensi rahisi na mambo mengine mengi ambayo ni ya msingi katika kujiendeleza kuongea Kiingereza sanifu. Amewaongoza wanaojifunza Kiingereza katika kitabu hiki kwa njia rahisi yenye kueleweka bila kutumia maelezo mengi. Pia ametumia misome halisi ambayo wasemaji wa lugha hii hutumia katika maongezi yao ya kila siku, ambayo hutoa utangulizi mkubwa wenye thamani ambao utaweza kukusaidia sana katika safari yako ya kujifunza kuongea lugha hii ya Kiingereza kwa ufasaha.
Read Less